Uza kwa sekunde
Chagua bidhaa, andika idadi, basi. Bei inajijaza, stoo inapungua yenyewe, na faida inaonekana papo hapo.
Rekodi mauzo kwa sekunde. Jua stoo iliyopo, madeni ya wateja na faida halisi kila siku, hata bila intaneti.
Rejareja na jumla, katoni, mifuko na vipande.
Mbegu, mbolea, dawa, pamoja na ruzuku ya mbolea.
Tofali, kalavati, nguzo: gharama halisi ya kila pc.
M-Pesa, Mixx, Airtel, benki: floti, kamisheni na hesabu ya jioni.
Chagua bidhaa, andika idadi, basi. Bei inajijaza, stoo inapungua yenyewe, na faida inaonekana papo hapo.
Ukipokea mzigo inaongezeka, ukiuza inapungua. Unapata onyo bidhaa ikikaribia kuisha.
Kila mteja aliyekopa, alicholipa na anachodaiwa, mpaka amalize.
Ripoti ya siku, wiki na mwezi kwa PDF, Excel au WhatsApp, kwa kubonyeza mara moja.
Ongeza muuzaji kwa namba ya simu na PIN. Unaona kila alichouza, hata ukiwa mbali.
Endelea kuuza mtandao ukikatika. Data inajituma yenyewe intaneti ikirudi, bila kupotea.




Anza na mwezi 1 bure. Ukiridhika, lipa kwa simu kila mwezi. Hakuna mkataba.
Maduka, pembejeo na wazalishaji
Mawakala wa M-Pesa, Mixx, Airtel na benki
Vibanda 2–5: TSh 6,000 kila kimoja · Vibanda 6+: TSh 5,000 kila kimoja
Unaweza kulipia miezi 3, 6 au mwaka mzima kwa mara moja. Data yako inabaki salama hata kifurushi kikiisha.
Fungua link ya Daftari Pro kwenye simu yako. Android: Chrome, kisha ⋮ → "Add to Home screen". iPhone: Safari, kisha kitufe cha Share → "Add to Home Screen". Ikoni ya Daftari Pro itakaa kwenye simu kama app nyingine.
Ndiyo. Unaweza kuuza na kurekodi bila mtandao. Intaneti ikirudi, kila kitu kinatumwa chenyewe. Unahitaji intaneti mara ya kwanza tu unapoingia.
Kwa simu (Mixx by Yas) kwa namba itakayoonyeshwa ndani ya app. Ukishalipa, andika msimbo wa muamala kwenye app, na kifurushi chako kinawashwa.
Ndiyo. Mwongeze mfanyakazi kwa barua pepe au kwa namba ya simu na PIN. Kila mauzo yanaonyesha nani aliyeuza.
Data inahifadhiwa kwenye mtandao (Google Firebase), na wewe na wafanyakazi uliowaruhusu tu ndio mnaoiona. Unaweza pia kupakua nakala yako wakati wowote.
App inaacha kupokea rekodi mpya mpaka ulipie, lakini data yako yote inabaki salama na unaendelea kuiona.
Fungua akaunti kwa dakika mbili, ongeza bidhaa zako, na uone faida yako halisi kesho asubuhi.